Breaking info: Ngoma Amwaga Wino timu ya Sauzi - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

June 27, 2017

Breaking info: Ngoma Amwaga Wino timu ya Sauzi






Donald Ngoma inaaminika ameamua
kuachana na soka la Bongo, badala yake anatimkia Afrika Kusini atakapojiunga na Polokwane alikosaini miaka mitatuWakati mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma, akitarajiwa kuwasili nchini leo kumalizana na ama klabu ya Yanga au mahasimu wao Simba, mchezaji huyo ni kama anachezea akili za miamba hao
wa soka baada ya taarifa za ndani kudai ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
Ngoma alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga, lakini pia mshambuliaji huyo alishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Simba na inasemekana ujio wake ilikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo msimu ujao.

Kwa mujibu wa Mtandao wa KickOff.com, imethibitika Mzimababwe huyo amekamilisha zoezi lake la usajili kwenye klabu hiyo, baada ya kuwa huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na mabingwa wa soka Tanzania Yanga
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();