Mainfo93 imekusogezea b aadhi ya viungo bora wakabaji kwa msimu uliomalizika wa 2016/2017
Himid Mao ( Azam)
Ndiye kiungo mkabaji bora kwa sasa hapa nchini, anaongoza kwa kupokonya mipira , Himid nyota wa Azam na timu ya taifa Tanzania, amekuwa mzuri kwenye kuilinda safu yake ya ulinzi isipatwe na madhara kwa kuzuia hatari zote, kiungo huyo amekuwa na nidhamu kubwa kwenye eneo hilo kuliko kiungo yeyote kwa sasa
Jonas Mkude (Simba)
Kiungo huyo amekuwa mzuri kwenye kupiga pasi fupi fupi na ndefu kwa usahihi bila kupoteza, Mkude amekuwa muhimili mkubwa ndani ya Simba katika eneo la
katikati hasa la ulinzi na kuifanya timu iwe kwenye usalama pindi ikiwa inashambuliwa mara kwa mara
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar)
Licha ya umri wake kuwa mkubwa ila bado nyota huyo alifanikiwa kuhimudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa asilimia kubwa tofauti na matarajio ya wengi, Nditi amekuwa imara kwenye utimamu wa mwili hasa ikitokea kwenye mipira ya kugombania dhidi ya timu pinzani
Kenny Ally (Singida United)
Amejiunga na Singida akitokea Mbeya City aliyoichezea msimu uliopita, Kenny ana sifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali, ni mzuri kwenye kusoma mchezo kwa haraka na kugundua udhaifu na ubora wa mpinzani
Ally Nassoro (kagera Sugar)
Nyota wa klabu ya Kagera amefanikiwa kucheza kwa ubora mkubwa kwenye eneo la kiungo mkabaji kila anapopewa nafasi kwenye eneo hilo, ana uweo wa kupiga pasi fupi na ndefu pia ni mzuri kwenye kukaba bila kufanya faulo hali kadhalika ana uwezo mkubwa wa kufunga, amemaliza na magoli zaidi ya matatu licha ya kucheza chini sana
Stephan Kingue (Azam)
Ukitaja wakata umeme kwenye Ligi msimu uliopita jina la Kingue haliwezi kosekana, alionesha umaridadi wake hasa kwenye mashindano ya Mapinduzi kabla ya kuumia, Kingue siyo mzuri sana kwenye kupiga pasi kama wengine ila ni shapu kwenye kufika kwenye tukio kwa haraka na kulizuia, pia ni mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu kutokana na kimo chake