STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART 22) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

June 10, 2017

STORY:MJUKUU WA MSUKULE (PART 22)

STORY:MJUKUU WA MSUKULE
PART{22}
MWANDISHI:Amani Zabranco
Saguda alipochungulia ndani ya ule mtungi,akaona kuna watoto wachanga,Yule bibi akasema kuwa zile maiti za wale watoto hutumika kuchukua mafuta yake amabayo hutumiwa na wachawi ili kuweza kupaa angani kwa kutumia ungo. Mara ghafra sauti za ajabu zikaanza kusikika kwenye kile chumba, Yule kikongwe akaanguka chini,saguda alipoona kikongwe akiwa anatapatapa pale chini saguda akakimbia kwa kasi kutoka
nje ya kile chumba, wapishi walipomuona saguda amekimbia ikabidi waingie kule ndani ili kujua nini kimetokea.
Wakamkuta Yule kikongwe akiwa chini huku sauti za mizimu zikitanda ndani ya kile chumba,Wapishi wakamshika mikono ili kumtoa nje ya kile chumba, walipomfikisha kwa nje akawaambia wamuachie ili ajaribu kutembea peke yake wakamuachia akaanza kutoka nje alipofika  nje akamuona saguda akiwa kasimama kwenye mlango huku akionekana kuwa na wasiwasi.
Yule bibi akamfuata saguda kisha akamuuliza kama hajaumia popote,saguda akajibu kuwa hamna kilicho muumiza. Kikongwe akamuambia saguda kuwa mizimu ilikasirika kutokana nakitendo cha kutoa siri za himaya, akaendelea kusema kua ilitaka kumuua ila bahati nzuri ikashindikana kutokana na umachachari katika kupambana  na mizimu , kikongwe akamuambia saguda kuwa sasa inabidi waende chini ya mbuyu kwa ajiri ya sherehe.

Lakini akamkumbusha saguda kuwa wakimpa nyama ya binadamu inabidi ageuze viganja vya mikono kwa nyuma kwa kua wachawi  huchukia sana kwa hiyo wataacha kumpa nyama akifanya hivyo. Walipofika chini ya ule mbuyu,Yule kikongwe akaenda kukaa pale mbele kwa mkuu wa wachawi kwa kuwa naye alikua na cheo kikubwaa ndani ya himaya ya gamboshi.

Mkuu wa wachawi akasema kwa sauti kubwa na nzito”wechu,wechuuuuuuuu!!, leo ni siku ya kupokea watu wa kafara na tutakula nyama huku tukifurahi”. Mkuu wa wachawi akasema “ni lazima kila mmoja aliyehudhuria hapa aonje na kutafuna nyama za watu”, ngoma zikaanza kupigwa na wacheza ngoma wakaingia katikati ili kuanza kutoa burudani, wakawa wanacheza nanyoka wakiwa wamewavaa shingoni huku wengine wakiwabusu wale nyoka.

Mara kwa upande wa kushoto alipokaa Yule mkuu wa wacahawi, saguda akamuona adui yake ambaye ni kisiki cha mpingo, saguda moyo ukawa unamuuma hasira zikamjaa aka………………{Usikose part23}
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();