STORY:MAPENZI YA DOT COM (EPISOD-1) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

September 19, 2017

STORY:MAPENZI YA DOT COM (EPISOD-1)


Sabra akiwa amekaa nje ya saloon ya kusukia wanawake,mara kwabali anamuona kijana mmoja sharobalo akiwa anapita barabarani. Sabra akastuka moyo akawa anamtolea jicho yule kijana, yule sharobalo naye kuona anatolewa jicho vile naye ikabidi asimame akatoa earphone alizokuwa ameweka masikioni huku aliskiliza wimbo wa seduce me. Sabra alipoona yule sharobalo anamuangapia,ikabidi aweke pozi zuri la kumvutia yule sharobalo sabra akawa anarembua jicho kama kuku mwenye nyege. Alikuwa kavaa kimini cha dhambarau akawa anatanua vimapaja ili kumpagawisha yule sharobalo. Sharobalo kuona vile naye akazidi kumtamani sabra kwa kuwa mapaja yake yalikuwa manene. Sharobalo mate yakazidi kukimbizana utazani mlevi kaona mshaki wenye pilipili ma limao. Sabra akanyanyua kiganja chake cha mkono akaonyesha ishara ya vidole kumuita yule sharobalo.

     Sharobalo kuona vile taratibu bila kulaza damu akaanza kujongea kuelekea pale alipokuwa amekaa sabra. Sharobalo ikabidi abadili mwendo akawa anatembea kwa mikogo mithiri ya basi la mwendokasi linapokaribia kupaki. Sabra jicho lote likawa kwa yule sharobalo,sabra akawa anahisi moyo wake ni mwepesi kama vile amemwagiwa barafu iliyoyeyuka.Sharobalo akafika hadi pale alipokuwa sabra.

Sharobalo akasema
"Mambo nini mrembo".

Sabra akajibu.
"Fresh tu! ila kunikompare na sinderela haiwezi kuwa fresh".

Sharobalo akatabasam akasema.

"Basi muruaaaa, kama vipi seduce me dada"

Sabra akachekaaaa kisha akasema
"Usiwaze ukitaka kiti nitakupa hadi kitanda ukalale".

Wote wawili wakawa wanafurahi kwa kuwa walikuwa wakiongea kwa furaha. Yule sharobalo ikabidi aulize.
"Samahani bi shosti waitwa nani vile???".

Yule binti akajibu
"mie naitwa sabra ila wengi wanapenda kuniita sabra mapozi".

Yule sharobalo akawa anafurahi akasema.
"Hahaaa hawajakosea kabisaa maana mapozi kama haya hayajawahi kumuacha mtu salamaaa".

Sabra akasema
"mh! me mbona wa kawaida tu, any way nawe unaitwaje???".

Sharobalo kwambwembwe akajibu
"Wanapendaga kuniita Bill Gates The Hacker".
Sabra akacheka:-D:-D akasema "hilo ndilo wazazi wako walokupa?????

Sharobalo akajibu
"aaaahhhh sabra kausha si unajua si ma down town huwa tuna majina yetu flani ya instagram, mbona wengine  ni kina bashite ila instagram wanajiita #KIPUSA #PASUA KICHWA

Sabra kicheko kikamshika akasema
"duuu kweli bhana wengine wanajiita kina #dangote #simba sa sijui chui atakuwa nani!!!".

Wakaendelea kuongea huku wakicheka kwa furaha, lakini kwa muda wa kama dakika mbili ukimya ukatawala, sabra akawa amekaa kwenye kiti kizuri cha kisasa chenye rangi ya pinki huku bill gates the hacker akiwa amekaa kwenye kiti cha kijivu.

Wote wawili wakabaki wanaangaliana machoni, sabra akaanza tena kumtega bill the hacker, akawa anatanua na kuchezesha mapaja taratibuuu, akawa anayachezesha hadi kile kimini kikawa kinazidi kupanda juu, mapaja yote yakawa live bila chenga.

       Bill the hacker akazidi kupagawa kwa kuwa mapaja ya sabra yalikuwa yaki meremeta utazani embe dodo lilopakwa mafuta. Sabra akawa analegeza jicho kwa hisia nzito za kimahaba, mara biil gates the hacker aka..........(ITAENDELEA, TUTAFUTE GOOGLE@ Mainfo93.com). #Zabranco.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();