STORY :MAPENZI YA DOT COM (SEHEMU YA 2 - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

September 21, 2017

STORY :MAPENZI YA DOT COM (SEHEMU YA 2


Sehemu  iloyopita iliishia pale sabra alipokuwa amekaa na bill the hacker. Wakapeana mawasiliano kisha bill akaondoka pale saloon, ilipofika usiku majira ya saa tatu sabra akampigia simu bill na kumueleza hisia zake.
Wote wawili wakawa wamekubaliana huku kila mmoja akimpenda mwenzake.
Sabra akamuuliza bill the hacker kuwa anafanya kazi gani,bill akamuambia kuw yeye ni software injinia.
Sabra hakuweza kuelewa chochote akamuuliza bill akajibu inahusiana na masuala ya mtandaoni pamoja na utaalamu wa computer.
Bill the hacker akamuambia sabra kuwa walimpa jina hilo kutokana na umahili wake katika kufanya udukuzi mtandaoni na huwa unampatia fedha nyingi ambazo ni dola za kimarekani pamoja na euro.
Bill nae akamuuliza sabra kuwa anafanya kazi gani. Sabra akajibu kuwa yeye ni msusi wa saloon ya kisasa ya wanawake.  Bill the hacker akamuambia kuwa atajitahidi ambadilishie kazi sabra.
  Sabra ndani ya moyo wake akawa anajiuliza itakuwaje kama atafanikiwa kupewa mtaji mkubwa na kuwa mjasiria mali mzuri
Wiki kadhaa zikapita huku bill na sabra wakiwa wapenzi na moto ukizidi kuangaza penzi lao,siku moja bill akamuita sabra aje nyumbani kwake.
Sabra akawa hana cha kusema akajiandaa na kwenda hadi kwenye jengo moja la ghorofa ambapo bill alikuwa kapanga room.
Alipofika chumbani kwa bill akawa anajisikia furaha kwa kuwa palikuwa pazuri sana,masofa ya kifahari, zuria zuri huku pembeni pakiwa na friji moja kubwa la kisasa.
Ndani ya kile chumba kulikua na sehemu ya mbele ambapo kuna computer sita kubwa kubwa zilizopangwa katika series.
  Mezani kulikuwa na laptop tatu za kifahari, Sabra akawa haamini anachokiona akasema.
"hapa nimeamini kwa nini watu wanakuita bill gates the hacker".
Bill akasema
"usijari sabra hapa ndipo kwangu na hii ndo ofisi yangu, to cut a chase hii ni home ofice".
Bill akamuambia sabra akae kwenye sofa kisha akasema.
"Leo nimekuita hapa nilitaka tupeane raha, ila kuna deal moja nimeipata mtandaoni muda huu, kuna pesa zinatumwa kupitia mtandaoni na shirika moja, zinatoka indonesia zinaenda brunei, hapa nipo nategesha program zangu ili nizinase na kuziweka katika akaunti zangu."
"Sabra akasema usijari baba, me nipo na wewe kwa kila hatua, hizo pesa ni kasi gani???"
bill akajibu ni..........(ITAENDELEA)
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();