HATIMA YA OKWI KUELEKEA GEM YA KESHO. - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

January 17, 2018

HATIMA YA OKWI KUELEKEA GEM YA KESHO.



Masoud djuma amefunguka hatima ya mchezaje wake, emanuel okwi kuelekea gem ya kesho dhidi ya singida united.


Djuma alisema, mshambuliaji huyo amefanya mazoezi vizuri kwa kufanya programu zote za kukimbia mbio fupi na ndefu kabla ya kuchezea mpira.

Aliongeza kuwa, Okwi kesho (leo) asubuhi atafanya mazoezi ya mwisho ya pamoja na wenzake kabla ya mchana kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro walipokwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida.

“Okwi amelirejea Dar jana (Jumatatu) na siku hiyo jioni alifika hapa mkoani Morogoro ambako tumeweka kambi kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida tutakayocheza kesho (Jumatano).

“Mara baada ya kufika leo (jana) alifanya mazoezi ya pamoja na wenzake kabla ya kesho (leo) Jumatano asubuhi kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya timu kurejea Dar kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida ambayo yeye anatarajiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji nitakaowatumia, hakika naamini kuwa huyu ni mchezaji muhimu na ataisaidia sana timu hii,” alisema Djuma.

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();