SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA(Sehemu ya 1) - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

October 03, 2017

SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA(Sehemu ya 1)

Story hii inahusu maisha ya familia ya watoto wanne ambao walikuwa hawajawahi kupata furaha maishani mwao kutokana na misuko suko ya maisha.

Simulizi inaanza, siku ya juma tano ikiwa ni majira ya saa kumi jioni. Mwanaume mmoja aitwaye selembe anaonekana akiwa anapita katikati ya  barabara huku akiwa amebeba mzigo mkubwa wa viazi begani kwake, lakini wakati anakatiza barabara mara vijana watatu wakiwa wamepakizana kwenye boda boda ghafra wakawa wanaendesha kwa kasi kubwa.
     Yule mwanaume alipostuka akaona wapo mbele yake kama sentimita tatu, macho yake yakawa kama vile yanaona nyota nyota. Boda boda ikampamia yule mwanaume, ikawa imemchana kifuani. kipande kingine cha chuma kikawa kimempitia katikati ya tumbo kikachanachana vibaya hadi utumbo ukamwagika chini.

     Damu ya yule mwanaume ikawa imeruka kwa kasi, matone yake yakawa yamerukia kwenye milango ya maduka ya pembezoni. Wale boda boda wakawa wametupwa ndani ya mtalo wa maji machafu, wakawa wamelowa matope yanayotoa harufu mbaya. Baadhi ya wasamalia wema wakawa wanawavuruta kuwatoa ndani ya yale maji.
   Walikuwa wameumia vibaya sana ikabidi wachukuliwe na kukimbizwa hospitali.
Bahati mbaya yule mwanaume aliyepamiwa akawa amekufa pale pale ikabidi taratibu za kuutoa mwili wake kuupeleka mochwari zifanyike.
  Wakati wanampakiza ndani ya gari mara watoto wa shule ya msingi wakawa wanatoka shuleni, wawili kati yao walikuwa ni watoto wa yule mwanaume. Wenzao wakawa wananong'onona.

     "baba yenu amegongwa na pikipiki!!!".

Wale watoto kusikia vile wakatupa madumu ya maji na fagio wakakimbia kulisogelea lile gari. Wakawa wanaita huku machozi yakiwatoka.

"babaaaaaaaa,babbaaaaaaaaa!!!"
Ghafra......(ITAENDELEA INGIA mainfo93.blogspot.com).

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();