SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA (Sehemu ya 3). - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

October 05, 2017

SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA (Sehemu ya 3).

MWANDISHI:AMANY ZABARANCO
SIMULIZI:CHOZI LA FUKARA
SEHEMU YA 3

Nesi akasema

"unalia nini sasa???,umeambiwa hii wodi ya watoto????".

Yule mwanamke akazidi kupata uchungu kwa kile alichoambiwa. Akasema

"Unanitusi???,mume wangu kapata ajari unanitusi????kumbuka hujafa hujaumbika".

Baada ya yule mama kuyasema maneno yale,  ndani ya kile chumba kulikuwa na daktari mwingine wa kiume ikabidi asogee na kumuuliza yule mama kuna tatizo gani, yule mama akajibu.

"mimi mume wangu kapata ajari ya bodaboda, sasa namueleza huyu ana nitusi!!".
Yule daktari akamuangalia yule nesi kisha akasema.

"mbona unakuwa na kauli mbovu??? huyu mama anakueleza unajibu nyodo!!!.tangulia ofisini kwangu ukaandike maelezo kwa ulichokifanya".

Nesi akaanza kutetemeka mikono huku anamungalia yule daktari kwa hofu kubwa

kisha yule daktari akasema
"jamani wateja tunaomba radhi kwa kilichotokea, kweli huyu mama yuko sahihi kuna mtu kaletwa hapa muda si mrefu,ameumizwa vibaya hadi utumbo upo nje pia kifua kimeachana, kwa hiyo msihisi huyu mama kawapita nyie bure bure".

Wote wakaitikia

"sawa muheshimiwa, ila tunaomba huyo jesi ashikishwe adabu".

Wakati wanaongea pale mara ghafra gari nne za kiserikali zikaingia pale hospitali,wakashuka wakaguzi.
Wakawa wanatembelea wodi moja baada ya nyingine wakafika hadi pale alipokuwa yule mama.

mkaguzi mmoja akasema

"Naitwa maiko manyama,natokea kituo cha maadili ya utumishi wa umma,tumekuja kukagua kama kuna utovu wa nidhamu kwa watumishi".

Watu waliokuwepo pale wakajibu

"Karibu sana mkuuu"

Mkaguzi akauliza

"jamani kuna tatizo lolote kwenye kituo???".

Wale watu wakaitikia
"Ndioo mkuuu sasa hivi hapa kuna nesi kamtukana huyu mama".

Mkakuzi akamuuliza yule mama kama ni kweli kinachosemwa,yule mama ikabidi asimulie jinsi ilivyokuwa. Yule mkaguzi akakasirika akageuka kumuuliza yule daktari

"Ni kweli kinachosemwa kimetokea???".

Daktari akawa anasita akataka kumtetea yule nesi lakini akakumbuka kuwa kilichotokea kimeshuhudiwa na watu wote ikabidi aseme

"ndio mkuuu jambo hili limetokea na nimemuamuru huyo nesi akaandike maelezo".

Mkaguzi akasikitika sana akasema
"Jambo hili halina mjadara hawezi kutesa wanyonge tukamfumbia macho, kwa mujibu wa ibara ya 6 kifungu kidogo cha 9 cha miiko ya utabibu naamuru nesi huyo afutwe kazi mara moja kuanzia hivi sasa".

Dakatari akapatwa na wasi wasi akawa anahofia na yeye asije kuadhibiwa.

Yule mkaguzi akamuangalia daktari akasema
"na wewe ulikuwa wapi wakati huu upuuzi unafanyika???".

Daktari akawa anapata wasiwasi kusema ukweli kwa kuwa alikua akisikia yale maneno. Wakati daktari anataka tu kusema wale watu waliokaa kwenye mabenchi wakamtetea wakasema.

"Hapana mkuu huyu hakuwepo alikuwa anatibu, huyu kijana ni mchapa kazi anatujari wagonjwa".

Mkaguzi akasema
"sawa nimewaaerewaaa, mimi ni mr.manyama sipendi ujinga kabisa, daktari usijari endelea kuchapa kazi".

Wakaguzi wakaamrisha walinzi waje kumtoa yule nesi,wakawa wana msindikiza. Nesi akawa analia huku anamuangalia yule mama akawa anakumbuka neno moja "kumbuka hujafa hujaumbika".

Yule mama akawa anamungalia yule nesi jinsi anavyo dharirika, neno moja likawa linamjia kichwani yule mama akawa anahisi kama mume wake anamuambia
"CHOZI LA FUKARA HUWA HALIMWAGIKI BURE!!".

Wale wakaguzi wakamuomba daktari awapeleke kumuona mume wa yule mama. Wakaongozana pamoja na yule mama hadi  kwenye chumba cha daktari,
Daktari akamuuliza yule mama

"unaitwa nani na mume wako anaitwa nani???".

Yule mama akajibu
"Naitwa malembeshi mume wangu ni sesembe".

Daktari akawa anasikitika kwa kuwa hilo jina alilotajiwa alilisikia wakilitaja.

Daktari akasema

"Malembeshi!!!"
Yule mama akaitika
"abeeee"

"Mume wako............(ITAENDELEA LIKE PAGE YETU #MAINFO93)
TUPE MAONI JE UREFU WA STORI UNARIDHISHA???

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();