SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA (sehemu ya 2). - MAINFO93

Latest

Kuwa updated kwa kutembelea mainfo93, hapa utakutana na mastory toka kila kona ya ulimwengu wa dot com. Contact habarimtandaoni@gmail.com

Random posts

October 04, 2017

SIMULIZI #CHOZI LA FUKARA (sehemu ya 2).

Mwandishi: Amany Zabranco.

Sehemu iliyopita iliishia pale wale watoto walipokuwa wakilikimbilia gari la maiti.

Sasa twende nayo

Watu ikabidi wawashike wale watoto ili wasije kulifikia gari,kila mmoja aliyekuwepo pale akawa anasikitika,wale watoto wakapelekwa nyumbani kwao.
Walipofika wakamkuta mama yao anaosha vyombo nje, yule mama akawa anashangaa kuwaona wanawe wanalia huku akiwa hajui kinachoendelea.

     Akawaambia
"Wanangu poleni kwa njaa najua jana usiku hatukula, baba yenu kaenda kuhangaika muda si mrefu ataleta unga,humu ndani umeisha".

Wale watoto ndio wakazidisha kulia baada ya maneno ya mama yao. Sasa ikabidi mmoja wa wale watoto wawili aseme

"Babaaaaa amegongwa na pikipiki!!".
Yule mama kusikia vile akastuka akaangusha kikombe cha udongo alichokuwa akiosha akabaki ameshika mikono kichwani akasema.

"jamanii mungu mi nimekosa nini mbele yakoo?????".

Ikabidi asimame haraka haraka akaingia ndani akachukua kanga akajifunga akatoka kwenda eneo la tukio,alipofika njiani majirani wakawa  wamemuita wakampa pole kisha wakamchangia kiasi kadhaa cha shilingi akachukua usafiri na kuelekea hospitali.

     Alipofika hospitali akakuta foleni ndefu ikabidi awapite watu wote akaenda hadi dirishani, kwa ndani kulikuwa na nesi wa kike. Alipomuona yule mama amewapita wengine,yule nesi wa kike akasema kwa dharau.

"khaaaaaaaa!!!!we mama vipi???,unawazimu???,umerogwa niniii wewe!!!".

Yule mama kusikia yale maneno chozi likaanza kumtiririka.

Nesi akasema........(ITAENDELEA LIKE PAGE YA MAINFO93 Uwe wa kwanza kuipata#by zabranco

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();