MSANII wa bongo Movie anayefahamika kwa jina la Suzan Michael ‘Prettykind’ aliyewahi kucheza filamu mbalimbali zikiwemo Damu Yangu, Who is back, apple na Uyoga yamemkuta mazito baada ya kurubuniwa na kupelekwa kuuzwa nchini India, Risasi Jumamosi limezungumza naye na kufunguka.
Chanzo Cha habari hii Awali chanzo chetu ambacho kipo nchini India kiliwasiliana na gazeti hili na kudai kuwa, binti huyo mrembo ambaye kwa sasa yuko Bongo alifukuzwa huko baada ya kugonganisha wanaume wawili raia wa Nigeria na kusababisha balaa kubwa
Nikajaribu kumuomba yule aliyekuwa akinisaidia anilipie zile pesa lakini haikuwezekana, sikuwa na njia tena zaidi ya kubaki kule. afunDishwa kila aina ya ulevi Katika kushawishiwa aiweze kazi ile ambayo hakuizoea, aliambiwa anywe pombe avute madawa ya kulevya na sigara ndiyo ataiweza lakini vilevi vyote hivyo alivikataa na kuamua kujiuza kawaida kwani hakuwa na namna ya kufanya ili aweze kurudisha pesa za watu. “Nilijiuza kwa wanaume wanne kwa siku ili tu nifanikishe kupata pesa za kumlipa yule dada haraka. Nikiwa kwenye mishe hizo nilikutana na mwanafunzi wa Kinigeria, aliponinunua nikamweleza matatizo yangu, akanisaidia kunilipia, nikawa najiuza kwake yeye tu
mpaka nikamaliza deni, tukaamua kuishi wote,” anasimulia. mwanafunzi aonDoka, amuaChia Chumba “Yule Mnigeria alipoondoka aliniachia chumba ikiwa bado mwezi mmoja tu kodi iishe, ikabidi nirudie kazi ile ya kujiuza ili nipate pesa ya kujikimu kwani maisha ya kule bila kazi hayaendi. “Katika kujiuza nikapata bwana mwingine mtu mzima ambaye alinichukua nikakaa naye na kuachana kabisa na kazi ya kujiuza mpaka narudi Tanzania kwani alinisaidia sana.” apata gonJwa baya Msanii huyo anaeleza kuwa, katika kujiuza huko alipata gonjwa baya la kuwashwa na kutokwa na uchafu sehemu za siri hali iliyomfanya akose amani kabisa.
“Nilihangaika hospitali zote na kupatiwa matibabu nikapona ikiwa ni pamoja na kupima Ukimwi ambapo nilikutwa salama, namshukuru Mungu.” afiChua siRi nzito Prettykind alieleza kuwa, kuna baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao wamekuwa wakienda India kuuzwa kwa siri na wakirudi wanatesa mjini. “Siwezi tu kuwataja lakini wapo mastaa ambao nilikutana nao kule, nao wakijiuza tena wakati mwingine kwa bei chee, hali ngumu sana.” atoa somo kwa mabinti wenye tamaa Mlimbwende huyo alisema, lengo la kusimulia mkasa huu ni ili mabinti wenye tamaa ya kutafuta mafanikio kwa njia ya haraka wapate fundisho kwani kilichompata yeye asingependa kimpate mwingine. “Ni suala la kila mtu kujitambua na kutambua thamani yake, usikimbilie maisha mazuri kwa njia ambazo ni hatari. Na katika hili nitafungua taasisi yangu ya kuwashauri wasichana wanaopitia maisha magumu kama yangu, nitapita mashuleni na kila sehemu kutoa ushuhuda wa maisha yangu ili liwe fundisho kwa wengine. neno la mhaRiRi Prettykind amesikika, iwe funzo kwa wasichana wote wanaopenda maisha kwa pupa.